Kutanguliza siku sita za Shawwaal kabla ya swawm ya kafara

Swali: Bwana mmoja anadaiwa kafara ya miezi miwili mfululizo na akataka kufunga swawm ya siku sita za Shawwaal. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Kilicho cha lazima ni yeye kuharakisha kufunga swawm ya kafara. Haijuzu kutanguliza swawm ya siku sita juu yake. Kwa sababu imependekezwa tu na kafara ni faradhi ambayo ni lazima kwa njia ya upesi. Kwa hivyo imelazimika kuitanguliza swawm ya kafara mbele ya swawm ya siku sita na swawm nyenginezo zilizopendekezwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/394)
  • Imechapishwa: 07/05/2022