Ameshindwa kukamilisha swawm ya Shawwaal kutokana na udhuru

Swali: Nilianza kufunga siku sita za Shawwaal lakini hata hivyo sikuweza kuikamilisha kutokana na baadhi ya mambo na kazi kwa vile nilibakiza siku mbili. Nifanye nini? Je, nizilipe? Je, napata dhambi kwa jambo hilo?

Jibu: Kufunga siku sita za Shawwaal ni ´ibaadah iliyopendekezwa na sio lazima. Kwa hivyo unapata thawabu kwa zile siku ulizofunga. Kunatarajiwa kwako kupata ujira kamili ikiwa kilichokuzuia kukamilisha ni udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtu anapokuwa mgonjwa au akasafiri, basi Allaah anamwandikia mfano wa aliyokuwa akiyafanya katika hali ya ukazi na uzima.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Hulazimiki kulipa yale uliyoacha.

[1] al-Bukhaariy (2996).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/395)
  • Imechapishwa: 07/05/2022