Kufunga siku ya kuzaliwa ya mtoto

Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto? Huku kwetu wanasema kuwa bora ni kufunga siku hiyo badala ya kusherehekea. Ni yepi ya sahihi?

Jibu: Sikukuu ya kuzaliwa au kufunga kwa sababu ya siku ya kuzaliwa yote hayo ni Bid´ah na hayana msingi. Hakika si venginevyo ni lazima kwa muislamu kujikurubisha kwa Allaah kwa yale aliyomfaradhishia na ´ibaadah zilizopendekezwa. Aidha awe katika hali zake zote ni mwenye kumshukuru na mwenye kumhimidi juu ya ile miaka yote inayompitia akiwa na afya njema.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (02/261) nr. (20834)
  • Imechapishwa: 07/05/2022