Kukusanya kati ya swalah mbili wakati wa vita

Swali: Je, kipindi cha vita kunakusanywa kati ya swalah mbili au kila swalah iswaliwe ndani ya wakati wake?

Jibu: Udhahiri ni kwamba kila swalah inaswaliwa katika wakati wake. Kwa sababu wakati wa kulinda mipaka ya nchi au wakati wa kuwapiga vita maadui kunapelekea kutenga wakati wake. Ikiwa swalah moja inatofautiana na swalah katika hali ya ukazi, kwa njia ya kwamba kikosi kikaswali Rak´ah moja na kikosi kingine kikaswali Rak´ah nyingine, kikosi kimoja kinalinda na kikosi kingine kinaswali. Hilo linapelekea swalah iwe moja peke yake. Vivyo hivyo swalah ya pili wataiswali kama swalah ya khofu. Kwa sababu wakiswali swalah mbili au wakakusanya swalah mbili itachukua wakati mwingi ilihali wanahitaji kujipanga dhidi ya adui.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 09/10/2021