Du´aa ya kufungulia swalah ni Sunnah katika faradhi na swalah za Sunnah

Swali: Baadhi ya maimamu wa misikiti katika Ramadhaan hawasomi du´aa ya kufungulia swalah katika Tarawiyh. Ni ipi hukumu ya kitendo chao hichi?

Jibu: Du´aa ya kufungulia swalah ni jambo limependekezwa katika faradhi na swalah za sunnah. Yule atakayeiacha hakuna neno juu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/74)
  • Imechapishwa: 09/10/2021