Swali: Ni ipi hukumu ya kutamka kwa sauti nia ya swalah?

Jibu: Kutamka nia ni Bid´ah. Kuidhihirisha kwa sauti ni dhambi zaidi. Sunnah ni kunuia kwa moyo. Kwani Allaah (Subhaanah) anajua siri na yaliyojificha. Yeye ndiye kasema:

قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّـهَ بِدِينِكُمْ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ

”Sema: ”Je, mnamfundisha Allaah juu ya dini yenu na hali Allaah anayajua yale yaliyomo mbinguni na yale   yaliyomo ardhini?”[1]

Haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mmoja katika Maswahabah wala kutoka kwa maimamu wanaofuatwa kwamba walitamka nia. Kwa hiyo ikatambulika kwa njia hiyo kwamba si jambo lililowekwa katika Shari´ah. Bali ni miongoni mwa Bid´ah zilizozuliwa.

[1] 49:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/423)
  • Imechapishwa: 09/10/2021