Kukojoa kwa kusimama na kujipangusa na kuta

Swali: Inajuzu kukojoa kwa kusimama na kujipangusa kwenye kuta ikiwa kuna maji?

Jibu: Ndio. Yote mawili yanajuzu. Inajuzu kukojoa kwa kusimama, lakini lililo bora zaidi ni kukojoa kwa kukaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya yote mawili. Alikojoa kwa kukaa, jambo ambalo alikuwa akifanya mara nyingi, na alikojoa kwa kusimama. Inasemekena ni kwa kuwa alikuwa mgonjwa na imesemekana kuwa alifanya hivo kwa sababu ya kuonesha kuwa inajuzu. Maoni haya ya pili ndio sahihi. Lakini hata hivyo anatakiwa kujilinda na cheche za mkojo zisimrukie.

Inapokuja katika kujipangusa, anaweza kujipangusa kwa kuta, mawe au kitu kingine chenye kuchukua nafasi ya mawe midhali kitu hicho kinasafisha na kukausha. Haina neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340204.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020