Swali: Swawm ya wajibu ambayo haikuwekewa kikomo cha wakati, kama mfano wa kafara na kulipa deni, ni lazima kuikamilisha au inafaa kukatisha swawm siku hiyo na kuifunga siku nyingine?

Jibu: Zingatieni jambo. Akifunga swawm ya wajibu, kama mfano wa kafara, kulipa deni la Ramadhaan au nadhiri, basi analazimika kwake kukamilisha siku hiyo. Haijuzu kwake kuikata swawm hiyo. Ni kama ambavo haifai kwake kukata swawm ya Ramadhaan. Haijuzu kufanya hivo. Kuhusu swawm inayopendeza inafaa kuikata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 29/04/2023