Amejilazimisha kumswalia Mtume idadi maalum

Swali: Ikiwa mtu atajilazimisha nafsi yake kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) idadi maalum kwa siku kwa mfano mara 2000 au mara 5000. Je, inazingatiwa ni katika Bid´ah?

Jibu: Ikiwa ameweka nadhiri basi atalazimika kutekeleza nadhiri yake kwa sababu ameweka nadhiri ya utiifu. Kama hakuweka nadhiri, basi amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kiasi atachoweza pasi na kuweka kikomo cha idadi maalum.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 29/04/2023