Kukariri jina la Allaah kwa idadi maalum

Swali: Katika mji wetu kuna ada ya baadhi ya watu wakati wanapomuomba Allaah wanasema “Ee Latwiyf”, “Ee Latwiyf”, “Ee Latwiyf” na wanaikariri mara nyingi na inaweza kufika mpaka mara mia moja. Je, inajuzu kuomba hivi?

Jibu: Ndio, huku ni kumuomba Allaah kwa jina miongoni mwa majina Yake. Lakini kule kuwa kwa sauti ya pamoja hii ndio Bid´ah. Ikiwa wanakariri hivo kwa sauti ya pamoja ni Bid´ah. Lakini lau mtu atakariri peke yake haina neno.

Jambo lingine ni kwamba hakuna idadi maalum. Kitendo cha kuweka mpaka ni kitu kinahitajia dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-6-8.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020