Swali: Ikiwa kuna mtu anayeendelea kufanya maasi, kama mvuta sigara au maasi mengine, nikamnasihi mara ya kwanza na kumkataza lakini akaendelea katika maasi yake. Je, nimeitakasa dhimma yangu kwa ile mara ya kwanza [kumkumbusha] au ni lazima kumnasi kila wakati?

Jibu: Ni lazima kila wakati unapoona anafanya maasi umnasihi. Usiwe kama mfano wa Banuu Israaiyl ambapo mmoja wao alikuwa akimkumbusha ndugu yake juu ya maasi kisha anamuona siku ya pili na ya tatu halafu anamuacha, anakaa naye, anakula naye na kunywa naye. Allaah Alipoona hivyo Akawalaani:

لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ

“Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israaiyl kwa lisani ya Daawuud na ‘Iysaa mwana wa Maryam. Hivyo ni kwa sababu ya [kuendelea] kuasi kwao na walikuwa wakipindukia mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya. Uovu ulioje waliyokuwa wakiyafanya.” (05:77-78)

Linalokupasa ni kumnasihi daima maadamu unamuona anafanya maasi usimuache. Ukiona kuwa hapokei nasaha usikae naye. Jitenge naye mbali.

Ama kuchanganyika naye, kukaa naye, kula naye na kunywa naye na huku unamuacha kwa madai ya kwamba umeshamnasihi na kumkumbusha, mpe nasaha maadamu uko pamoja naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-16.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020