Ni lazima kuleta tawbah kwa madhambi makubwa na madogo

Swali: Tawbah ya kweli inakuwa kwa madhambi makubwa tu au hata madhambi madogo pia? Je, madhambi madogo inatosha kwa mtu kuleta tu Istighfaar na kutenda matendo mema?

Jibu: Ni lazima kwa mtu kuleta tawbah kwa madhambi yote, sawa makubwa na madogo. Ikiwa hutubu kwa madhambi madogo yanageuka kuwa makubwa. Ni juu yako kuleta tawbah juu ya madhambi yote. Usichukulie wepesi kwa madhambi madogo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-5-16.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020