3169- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nimemuona Mola wangu katika sura nzuri kabisa. Akasema: ”Ulimwengu wa juu unazozana juu ya kitu gani?” Nikasema: ”Sijui.” Akaweka kiganja Chake cha mkono kati ya mabega yangu… ”

Hadiyth imepokelewa kupitia njia nyenginezo. al-Bukhaariy na at-Tirmidhiy wamesahihisha baadhi yake. Ndani yake zinasema kuwa hayo yalitokea kwenye ndoto, jambo ambalo linazidi kutilia nguvu kwamba ziada hiyo ni dhaifu. Zinduka juu ya hilo na rejea baadhi ya njia hizo katika ”Dhwilaal-ul-Jannah”[1].

Ibn-ul-Jawziy amechanganya mchanganyo wa kushangaza kati ya Hadiyth hizi ambazo ni Swahiyh ambazo unazozana ulimwengu wa juu (na katika baadhi yake imekuja ya kwamba ni ndoto) na Hadiyth nyenginezo zilizozuliwa ambazo zinasema kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola wake huko Minaa akiwa na rangi ya fedha juu ya ngamia na nyenginezo zilizotungwa[2]. Amefuatwa kichwa mchunga na Jahmiy kindakindaki kwa jina Hasan as-Saqqaaf alipokuwa anakiwekea taaliki kitabu chake ”Daf´ Shubah-it-Tashbiyh”.  Kitabu hicho adh-Dhahabiy alitamani lau asingelikiandika kwa sababu ndani yake kuna upindishaji wa sifa za kiungu unaofanywa na Mu´attwilah. Ibn-ul-Jawziy amefikia mpaka kusema kwamba Allaah hayuko ndani ya ulimwengu wala nje yake. Allaah, ambaye amelingana juu ya ´Arshi kulingana ambako kunaendana na utukufu na ukubwa Wake, ametakasika kutokamana na ´Aqiydah hii!

[1] Dhwilaal-ul-Jannah (388, 465 na 471).

[2] Nimetaja baadhi yake katika ”adh-Dhwa´iyfah” (6330).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naasir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/504)
  • Imechapishwa: 19/08/2020