Swali: Maneno ya Allaah (Ta´ala):

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ

“Je, mnadhani mko [katika] amani na Aliyeko mbinguni [juu]… ” (67:16)

Tumetangulia kusema ya kwamba ni miongoni mwa dalili zenye kuonesha kuwa Allaah Yuko juu ya viumbe Vyake. Vipi kumraddi mwenye kusema maana ya:

فِي السَّمَاءِ

“… Aliyeko mbinguni [juu]… ” (67:16)

bi maana ufalme Wake na Uwezo Wake?

Jibu: Haya ni maneno yake kwa mujibu wake yeye. Ama Kauli ya Allaah Amesema kuwa Yuko mbinguni.

وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَـٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَـٰهٌ

“Na Yeye ndiye mwabudiwa wa haki mbinguni na ardhini  mwabudiwa wa haki.” (43:84)

bi maana mwenye kuabudiwa mbinguni na katika ardhi. Allaah Amelingana juu ya ´Arshi. ´Arshi ndio kiumbe kilicho juu ya viumbe vyote.

وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً

“Naye ndiye Mshindi mwenye kudhibiti juu ya waja Wake na anakutumieni Malaika wanaohifadhi.” (06:61)

Wanachuoni wanasema dalili zenye kuthibitisha kuwa Allaah Yuko juu ya viumbe Vyake zimefika kiasi cha elfu. Haafidhw adh-Dhahabiy amekusanya nyingi katika dalili hizo kwenye kitabu chake “al-´Uluw lil-´Aliyy al-Ghaffaar”. Ama kujitokeza mtu na kusema ya kwamba maana yake ni kwamba mbinguni kuna ufalme wake na Malaika wake, haya ni maneno ya kipuuzi. Ni maneno yake yeye. Hayakubaliwi.

Swali: Anakufuru mwenye kupinga Allaah kuwepo juu ya viumbe Vyake?

Jibu: Hili halina shaka. Mwenye kusema ya kwamba Allaah Yuko pamoja na viumbe Vyake kwa Dhati Yake Amechanganyika nao, huyu ni Huluuliy. Haya ni madhehebu ya Huluuliyyah na ni kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall). Ni kufuru kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-6-8.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020