Bora asimamishiwe adhabu au aisitiri nafsi yake?

Swali: Mwenye kufanya kitu katika machafu kisha akatubu kwa Allaah, hali yake ikanyooka na akajifunza elimu kutoka kwa wanachuoni. Je, bora kwake ni yeye kuitakasa nafsi yake kwa kusimamishiwa adhabu?

Jibu: Hapana. Aisitiri nafsi yake. Tawbah inatosha. Midhali Allaah amemsitiri basi na yeye aisitiri nafsi yake. Tawbah inatosha na himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (107) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatoulahfan-22-06-1441.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020