Swali: Kanda ya Qur-aan inazingatiwa ni kama Qur-aan katika kuingia nayo chooni na kwenginepo?

Jibu: Haina hukumu moja [kama ya msahafu]. Lakini kutoingia nayo chooni ndio bora zaidi. Kuacha kuingia na kitu kilichoandikwa jina la Allaah, Tasmiyah au Aayah ni bora. Hata hivyo haina hukumu moja kama ya msahafu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22256/حكم-دخول-الخلاء-بشريط-القران
  • Imechapishwa: 20/01/2023