Swali: Je, inafaa kumlaani kafiri maalum? Je, kuna tofauti kati ya aliye hai na ambaye ameshakufa?

Jibu: Hapana. Alaani kwa njia ya ujumla. Awalaani mayahudi, manaswara na makafiri wengine kwa njia ya kuenea. Isipokuwa kafiri ambaye anawaudhi waislamu. Mtawala akiona alaaniwe basi hapana vibaya ikiwa anawaudhi kwa mapigano au kuwapa dhiki. Kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivowalaani kikosi cha watu wa Makkah; kama vile Abu Jahl na ´Utbah bin Rabiy´ah wakati walipowaudhi waislamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22258/هل-يجوز-لعن-الكافر-المعين
  • Imechapishwa: 20/01/2023