Swali: Mimi husimama kuswali katika masiku ya Ramadhaan baada ya kumaliza kuswali Tarawiyh na hurudi nyumbani kusoma Qur-aan na kuswali tena mpaka wakati wa swalah ya Fajr siku ya pili. Hujiambia mwenyewe kuswali Rak´ah mbili kwa ajili ya kumtii Allaah (Ta´ala) na kusema “Allaahu Akbar”. Hufanya hivi usiku kutwa mpaka inapomalizika Ramadhaan. Je, kitendo changu hichi ni sahihi?

Jibu: Kuhusu katika yale masiku kumi ya mwisho hapana vibaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiyahuisha ndani ya Ramadhaan kwa kufanya ´ibaadah na (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaamsha familia yake. Kuhusu zile siku ishirini za mwanzo bora kwako usikeshe. Bali lala sehemu ya usiku ili ujisaidie kwa kulala kwako juu ya familia yako na kazi yako ya mchana. Kwa maana nyingine swali yale aliyokuwekea Allaah katika Shari´ah pamoja na waislamu katika misikiti kisha baadaye ulale. Kuhusu yale masiku kumi ya mwisho inapendeza kuyahuisha kwa kusoma Qur-aan na kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/8579/فضل-العشر-الاواخر-من-رمضان-على-بقية-الليالي
  • Imechapishwa: 19/03/2023