Imekusanya:

1 – Kuamini kwa kukata juu ya uwepo wa Allaah, kwamba yuko juu ya viumbe, kwamba yuko juu ya ´Arshi kwa dhati Yake, kwamba amelingana juu ya ´Arshi kulingana kunakoendana na utukufu na ukubwa Wake, kwamba Yeye (Subhaanah) ndiye Mola wa walimwengu, kwamba ndiye Muumba wa kila kitu, Mwenye kumruzuku kila aliye hai na Mwenye kuhuisha na kufisha, Mwenye kuyaendesha mambo, kwamba ndiye Mwenye kusababisha sababu zifanye kazi, Mwenye kuteremka mvua, kwamba ndiye Mwenye kuteremsha mvua, kwamba Yeye (Subhaanah) ndiye Mola wa mbingu saba na Mola wa ´Arshi tukufu, kwamba ndiye Mwenye kudhalilisha jua, mwezi na nyota, kwamba ndiye anamiliki kusikia na kuona, kwamba ndiye Mwenye kuwafikisha na kumwongoza amtakaye kwa neema na fadhilah Zake, Mwenye kumpotosha amtakaye kwa uadilifu na hekima Yake, kwamba anafanya atakacho na anahukumu akitakacho pasi na kuulizwa kwa yale ayafanyayo lakini wao wataulizwa. Hii ndio ile iitwayo Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 07
  • Imechapishwa: 20/03/2023