03. Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat na maelezo yake

2 – Kuamini kwa kukata na kusadikisha ya kwamba Allaah yuko na majina mazuri na sifa tukufu na kuu. Majina hayo Mola amejiita nayo Mwenyewe au amemuita nayo Mtume Wake, na Mola amejisifu kwayo au amesifiwa kwayo na Mtume Wake. Mfano wa majina hayo ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, Mjuzi, Muweza, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu. Mfano wa sifa hizo ni ujuzi, uwezo, huruma, kuridhia, kughadhibika na nyenginezo. Ni lazima kuitakidi na kuamini kuwa majina na sifa hizi ni za kikweli. Ni sifa za kikweli ambazo zinalingana na utukufu na ukubwa Wake. Kwa maana nyingine hazilingana na majina na sifa za viumbe. Ni sifa na majina ya kweli. Kwa msemo mwingine haitakiwi kuzipotosha, kuzikanusha, kuzifanyia namna wala kuzilinganisha. Hivi ndivo anavyopwekeshwa Mola kwa majina na sifa Zake. Hii ndio huitwa Tawhiyd-ul-Asmaa´ was-Swifaat.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 07-08
  • Imechapishwa: 20/03/2023