3 – Kuamini kwa kukata na kusadikisha kwamba Allaah (Ta´ala) pekee ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa aina zake zote, kwamba ni lazima kumpwekesha Allaah kwazo na kulazimiana na jambo hilo na kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na swalah, zakaah, swawm, hajj, maombi, kuchinja, kuweka nadhiri, kutaka msaada, kutaka uokozi, kutufu, jihaad, kuwatendea wema wazazi, kuwaunga ndugu, kuwafanyia wema wazazi, kisomo cha Qur-aan na Dhikr kukiwemo kusema ”Subhaan Allaah”, ”Laa ilaaha illa Allaah” na ”Allaahu Akbar”, kuamrisha mema na kukataza maovu, kujizuilia na mambo ya haramu, kuwafanyia watu wema, kuwa na tabia njema, kujizuilia kuwadhuru na aina nyenginezo za ´ibaadah hali ya kufanya au kuacha. Huku ndio kumpwekesha Mola kwa matendo ya waja. Hii ni haki ya Allaah inayowalazimu waja Wake na wameumbwa kwa lengo hilo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

“Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.”[1]

Mitume wametumwa kwa lengo hilo:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”[2]

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut.””[3]

[1] 51:56

[2] 21:25

[3] 16:36

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 08-09
  • Imechapishwa: 20/03/2023