Kuhifadhi au makhitimisho mengi ndani ya Ramadhaan?

Swali: Kwa mnasaba wa kukaribia mwezi wa Ramadhaan uliobarikiwa; ni kipi bora kwa mtu ajishughulishe kuhifadhi na kuirejea Qur-aan au kusoma Qur-aan kwa wingi?

Jibu: Kinachonidhihirikia – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – katika uongofu wa Salaf ni kusoma Qur-aan kwa wingi na kupupia kukariri makhitimisho yake. Kwa sababu hiyo ni fursa. Sambamba na hilo mtu azingatie na aielewe. Anaweza pia kuongezea kuhifadhi kile atachoweza katika miezi mingine kwa ajili ya kukusanya kati ya manufaa mawili. Asome Qur-aan kwa wingi na atenge wakati mwingine kwa ajili ya kuhifadhi kile kitachomuwepesikia. Hili ndio bora zaidi. Kwa sababu mtu anatakiwa kusoma kwa wingi ili afanye makhitimisho mengi kwa ajili ya kuwaigiliza Salaf (Rahimahumu Allaah) na kutumia fursa. Isitoshe kufanya hivo ni kujifunza elimu na kuielewa dini. Hakika katika kusoma Qur-aan mtu anaielewa dini na kujifunza elimu. Kitabu cha Allaah ndani yake kuna uongofu na nuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2974/هل-يجمع-برمضان-بين-الحفظ-وكثرة-الختم
  • Imechapishwa: 29/03/2023