Kuhifadhi, kurejelea au makhitimisho mengi ndani ya Ramadhaan?

Swali: Ni lipi bora katika Ramadhaan; kuisoma Qur-aan, kuirejea au kuihifadhi?

Jibu: Mwanafunzi anatakiwa kukusanya yote mawili; asome Qur-aan, aisome kwa wingi na kuhifadhi akutengee sehemu katika wakati, arejee kile kitachomtatiza kwa mazingatio na arejee tafsiri ya Qur-aan. Afanye hivo ili kukusanya manufaa yote mawili. Kurejea tafsiri ya Qur-aan au kuhifadhi kile kitachomuwepesikia kusimshughulishe kutokana na kuisoma Qur-aan. Kwani hii ni fursa. Mwezi huu mtukufu ni fursa. Allaah atufikishe sisi na nyinyi kuweza kuifunga na kusimama kuswali hali ya kuwa na imani na kutaraji malipo. Ni fursa ya kusoma Qur-aan. Kwa ajili hiyo Salaf walikuwa wakielekea kusoma Qur-aan na wakiacha masomo na duara za kielimu. Lakini katika faida, manufaa na mambo yatayokusaidia kusoma Qur-aan ni wewe kurejelea vitabu vya tafsiri ya Qur-aan yale ambayo pengine yanakutatiza wakati wa kisomo ili ukusanye kati ya usomaji wa Qur-aan, kufahamu na elimu. Ukitenga sehemu ya wakati wako kwa ajili ya kuhifadhi kile kinachokuwepesikia katika hayo, basi hilo ni jambo linalotakikana na zuri. Kwa sababu mtu anatakiwa kuchuma ndani ya wakati wake. Huu ni wakati mtukufu na ndani yake kuna uchangamfu na nafasi ya kusoma na kufadhi yote mawili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/20994/هل-التلاوة-برمضان-افضل-ام-الحفظ-والتفسير
  • Imechapishwa: 29/03/2023