Daku ya mwanzoni mwa usiku

Swali: Mwenye kula daku mwanzoni mwa usiku kisha kabla ya adhaana ya Fajr akanywa maji na akala tende.

Jibu: Amefikia malengo.

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa kalenda haiko sawa na hivyo inafaa kula dakika 5 au 10 baada ya adhaana.

Jibu: Mtu anatakiwa kuchukua tahadhari. Muumini anatakiwa kuchukua tahadhari.

Swali: Maneno yake mtunzi yanajulisha kuwa kujizuilia ilikuwa baada ya adhaana?

Jibu: Ndio, anatakiwa kujizuia kabla ya asubuhi. Imekuja katika upokezi mwingine:

“Kiwango cha kusomwa Aayah khamsini kati ya adhaana na daku.”

Imekuja tena katika upokezi mwingine:

“Kati ya daku na swalah.”

Ninachotaka kusema ni kwamba ale na anywe mpaka kupambazuke kwa asubuhi. Kama alivosema (Jalla wa ´Alaa):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]

Kula na kunywa inakuwa mpaka mwishoni mwa usiku.

[1] 02:187

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23680/ما-وقت-السحور-وما-يحصل-به-فضله
  • Imechapishwa: 29/03/2023