Ibn Baaz kuhusu du´a iliyoenea wakati wa kukata swawm

Swali: Baadhi ya watu wakati wa adhaana wanasema:

اللهم لك صمت وعلى رزقك افطرت

“Ee Allaah! Nimefunga kwa ajili Yako na nimefuturu kwa riziki Yako.”

Jibu: Kumepokelewa juu ya hilo Hadiyth dhaifu. Lakini hapana vibaya akisema hivo. Hata hivyo sio Hadiyth Swahiyh. Ni dhaifu. Lakini maana yake ni sahihi. Amefunga na kufungua kwa ajili ya Allaah. Licha ya hivo mtu asione kuwa kusema hivo ni Sunnah. Aina ya du´aa hiyo ni Sunnah. Aina ya du´aa kwamba umefungua [kwa ajili ya Allaah] ni Sunnah na kuna matarajio ya kukubaliwa.

Swali: Kabla ya adhaana ya Fajr?

Jibu: Wakati wa kukata swawm na wakati wote wa funga yake. Hapana vibaya akisema hivo. Hata hivyo sio Sunnah ijapo inafaa kusema hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25431/ما-صحة-قول-اللهم-لك-صمت-عند-فطر-الصاىم
  • Imechapishwa: 29/03/2023