Kuharakisha hedhi ndani ya eda kwa anayechelewa kupata

Swali: Kuna mwanamke ameachika talaka rejea. Ada yake ya mwezi si yenye kudhibitika na inampotea. Ni ipi hukumu ya kutumia dawa za kuishusha pamoja na kuzingatia kwamba hivi sasa yuko ndani ya eda?

Jibu: Muda wa kuwa anapata ada ya mwezi akae eda kwa mujibu wa hedhi. Asitumie dawa za kuishusa damu yake. Akae eda kwa mujibu wa hedhi pale itakapokuja. Hedhi tatu. Asubiri itapokuja hata kama itachelewa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (01)
  • Imechapishwa: 01/02/2024