Swali: Nilipatwa na jeraha kwenye kidole gumba cha mguu wangu kikaoza na nikaingizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji. Kidole hichi kiliendelea katika hali hii kwa miezi sita bila ya kupona. Madaktari wanabadili bendeji siku baada ya nyingine na wamekifunga bendeji. Kila nilipokuwa natawadha nafuta juu ya kidole hicho. Je, kufuta kunatosheleza kutokamana na Tayammum? Maji yanafika maeneo yote ya wudhuu´ mbali na kile kidole kilichofungwa pamoja na kuzingatia kwamba bendeji inapofungwa juu ya dawa hakutoki kitu.

Jibu: Hapana shaka kwamba kufuta juu ya bendeji kunatosheleza kutokamana na Tayammum. Mtu akifuta juu ya bendeji ambayo iko juu ya kidonda wakati wa kuosha mguu ulio na kidonda kunatosha. Katika hali hiyo hakuna haja ya kufanya Tayammum. Hili ndio la wajibu kwake mtu anapokuwa na kidonda ambacho kina bendeji. Mtu anatakiwa kufuta juu ya bendeji yote na kunamtosheleza kuosha mguu wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4690/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D8%AD-%D8%B9%D9%84%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D8%A8%D9%8A%D8%B1%D8%A9-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%88%D8%B6%D9%88%D8%A1
  • Imechapishwa: 27/03/2020