Namna ya kuitikia salamu ndani ya swalah

Swali: Nikiwa naswali swalah ya Dhuhr ambapo nikatolewa salamu na mwengine niitikie au hapana? Ni kipi bora zaidi kwa yule mwenye kuingia?

Jibu: Ama kuitikia kwa kuongea haifai. Kwa sababu ukiitikia kwa kuongea swalah yako inaharibika. Ama kuhusu kuitikia kwa ishara hakuna neno. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiitikia salamu kwa ishara ambapo ananyanyua mkono wake ikiwa ni ishara ya kwamba nimesikia. Lakini hata hivyo siongei kwa sababu niko ndani ya swalah. Lakini ikiwa yule aliyetoa salamu atabaki mpaka akamaliza kuswali yule mwenye kuswali atamuitikia kwa kuongea. Ikiwa ataondoka basi ile ishara itatosha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1634
  • Imechapishwa: 27/03/2020