Swali: Je, inafaa kwetu kufunga siku ya ´Aashuuraa´ ikikutana na jumamosi?

Jibu: Hapana vibaya mtu kufunga jumamosi kwa hali zote. Ni mamoja katika swawm ya faradhi na inayopendeza. Hadiyth inayokataza kufunga jumamosi ni dhaifu na inayotofautiana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Kwa hiyo hapana vibaya kwa muislamu kufunga jumamosi. Ni mamoja swawm hiyo ni ya faradhi au ya kujitolea. Haijalishi kitu hata kama ataipwekesha. Hadiyth inayosema mtu asifunge jumamosi isipokuwa tu kama ni swawm ya faradhi sio Swahiyh. Bali ni dhaifu na inayopingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15475/جواز-صوم-يوم-السبت-مطلقا
  • Imechapishwa: 20/07/2023