Kulipa siku za Ramadhaan siku ya ´Arafah, ´Aashuuraa´ na masiku meupe

Swali: Je, mtu akifunga siku ya ´Aashuuraa´, siku ya ´Arafah na swawm ya masiku meupe zinasihi kutokana na yale masiku aliyokula [katika Ramadhaan]?

Jibu: Akizifunga kwa nia, akafunga siku ya ´Aashuuraa´, siku ya ´Arafah na masiku meupe kwa nia ya zile siku anazodaiwa, zinatosheleza. Kwani hakika si vyenginevyo kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6542/حكم-صيام-يوم-عرفة-والايام-البيض-وعاشوراء-قضاء
  • Imechapishwa: 20/07/2023