Anakufuru mwanamke wa Kiislamu anayeolewa na kafiri?

Swali: Mwanamke akiolewa na mwanaume kafiri na yeye anajua jambo hilo. Je, anakufuru kwa jambo hilo?

Jibu: Hapana, hakufuru. Lakini ndoa haisihi. Hata hivyo kama anaona kuwa kitendo hicho ni halali na akasema kuwa ni halali kwa mwanamke wa Kiislamu kuolewa na mwanaume kafiri, hapo ndipo anakufuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 20/07/2023