Swali: Kuna maswali mengi yanauliza juu ya kuwaoa wanawake wa Kitabu. Je, manaswara na mayahudi waliyopo hii leo wanazingatiwa ni katika watu wa Kitabu?

Jibu: Hapana shaka. Ni katika watu wa Kitabu kwa sababu wanajinasibisha na Kitabu. Allaah amewaita kuwa ni watu wa Kitabu licha ya kwamba anajua hali yao. Kwa hiyo watabaki kuwa ni watu wa Kitabu mpaka kisimame Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (37)
  • Imechapishwa: 20/07/2023