Kufunga siku sita za Shawwaal baada ya kumalizika mwezi wa Shawwaal

Swali: Mwanamke alipata ada yake ya mwezi ndani ya Ramadhaan kisha akalipa siku zake. Baada ya hapo akafuatisha siku sita za Shawwaal. Je, anapata ujira kwa jambo hilo?

Jibu: Alizifunga ndani ya Shawwaal?

Swali: Hapana, kwa sababu Shawwaal ilimalizika na hakuwahi kufunga siku sita za Shawwaal.

Jibu: Mwezi wa Shawwaal ukimalizika hakuna tena swawm. Wakati wake unakuwa umemalizika. Lakini afunge siku tatu za kila mwezi au afunge jumatatu na alkhamisi ya kila mwezi. Zote hizi ni kheri. Fadhilah za Allaah ni pana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23342/حكم-قضاء-ست-شوال-بعد-انتهاء-شوال
  • Imechapishwa: 29/12/2023