Ni kiburi kukaa kwa kuweka mguu juu ya mgu mwingine?

Swali: Baadhi ya watu wanazingatia kuwa ni kiburi mtoto kuweka mguu juu ya mguu mwingine mbele ya baba yake au mbele ya mwanachuoni.

Jibu: Hapana vibaya kuweka mguu juu ya mguu mwingine.

Swali: Kwa hiyo sio katika kuburi?

Jibu: Sio katika kiburi.

Swali: Mtu ameketi kwenye kiti na akaweka mguu wake juu ya goti lake?

Jibu: Hapana neno ikiwa haionekani sehemu yoyote ya siri yake. Mkao kama huo hauna neno kwa sharti isionekane sehemu yoyote ya siri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23343/هل-وضع-الرجل-على-الرجل-من-التكبر
  • Imechapishwa: 29/12/2023