Swali: Kuna mtu ana mazowea ya kufunga yale masiku matatu meupe kila mwezi. Masiku matatu ya mwezi alikuwa amesafiri. Je, atakaporejea afunge masiku matatu haya mwisho wa mwezi wa Sha´baan?

Jibu: Sio lazima. Ni Sunnah umepita wakati wake. Hata hivyo ni sawa akizifunga katika masiku mengine yaliyobaki. Hakuzifunga kwa ajili ya Ramadhaan. Amezifunga kwa sababu amezowea kufunga siku tatu katika kila mwezi. Hakuna neno. Ni kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili, isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”

Ikiwa alikuwa na mazowea ya kufunga siku tatu na akaikosa na baadaye akapenda kuifunga ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22394/حكم-الصوم-اخر-شعبان-لمن-فاته-صوم-اعتاده
  • Imechapishwa: 16/03/2023