Pindi imamu anaporefusha kisomo katika Rak´ah ya tatu na ya nne

Swali: Mswaliji katika Rak´ah mbili za mwisho katika swalah ya ´Aswr au ´Ishaa au katika Rak´ah ya mwisho ya swalah ya ´Ishaa pindi imamu anaporefusha bora anyamaze baada ya al-Faatihah au asome?

Jibu: Akisoma ni sawa. Bora – Allaah ndiye mjuzi zaidi – asome. [Abu Bakr] as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akisoma baada ya Rak´ah ya tatu katika Maghrib:

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا

“Ee Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu.”[1]

Makusudio ni kwamba imamu wake anaponyamaza kabla ya kwenda katika Rukuu´ asome kile kitachomuwepesikia.

Swali: Lakini bora kwa imamu kuleta Takbiyr hali ya kurukuu?

Jibu: Ndio.

[1] 03:08

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22392/ماذا-يفعل-لو-اطال-الامام-في-الثالثة-والرابعة
  • Imechapishwa: 16/03/2023