Swali: Kuna mtu amewahi Rak´ah moja pamoja na imamu ilihali ni msafiri. Je, akamilishe swalah kama Dhuhr au kwa kufupisha?

Jibu: Aswali ijumaa. Aswali Rak´ah nyingine ya pili. Linamuhusu yeye na mwingine. Yule mwenye kuwahi Rak´ah moja ya swalah ya ijumaa ataongezea juu yake nyingine. Ni mamoja ni msafiri au mkazi. Itasihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22390/ماذا-يفعل-المسافر-اذا-ادرك-ركعة-من-الجمعة
  • Imechapishwa: 16/03/2023