Swali: Kuna bwana mmoja msichana wake aliachwa na mume wake na mume wake alikuwa mlevi. Je, inafaa kwangu kuwatadharisha watu kutokana naye pasi na watu kuniuliza au ni lazima waniulize?

Jibu: Akitakwa ushauri basi atoe ushauri. Miongoni mwa nasaha ni amnasihi huyo aliyekuwa mume wake pia. Lakini ikiwa anadhihirisha maasi hana usengenyi juu yake uliokatazwa. Ikiwa anakunywa pombe sokoni au kwenye vikao vya kahawa pasi na kujali, basi hakuna usengenyi juu yake uliokatazwa.

Swali: Ni mwenye kujisitiri.

Jibu: Pengine akapokea nasaha akimshauri.

Swali: Kwa hivyo haijuzu kwake kusema juu yake chochote?

Jibu: Hapana. Huko ni katika kusengenya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22389/هل-يجوز-التحذير-من-السكير
  • Imechapishwa: 16/03/2023