Kafara kwa aliyejamii mara tatu mchana wa Ramadhaan

Swali: Kuna mtu amemjamii mke wake mara tatu katika mchana wa Ramadhaan. Je, analazimika kutoa kafara tatu au kafara moja tu?

Jibu: Kila siku moja ina kafara yake. Analazimika kutoa kafara tatu pamoja na kutubia. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Je, haitoshi kutoa kafara moja?

Jibu: Hapana, kila siku ina kafara yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22396/هل-تتعدد-كفارة-الجماع-في-رمضان-اذا-تكرر
  • Imechapishwa: 16/03/2023