Kufuata misikiti ya mbali kwa ajili ya kumswalia maiti

Swali: Baadhi ya ndugu hufuata misikiti ambayo wanaswalia jeneza. Wengine wakawakemea kwa hoja kwamba Salaf hawakuwa wakifuatafuata jeneza. Ni yepi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Ukemeaji hauna mashiko muda wa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekokoteza kuswalia jeneza. Ikijulikana kuwa kuna msikiti fulani ambao kuna jeneza na akaenda kumswalia, analipwa thawabu juu yake. Amekusudia kuswalia jeneza, jambo ambalo amelisisitiza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23654/حكم-تتبع-المساجد-التي-فيها-جناىز
  • Imechapishwa: 12/03/2024