Kuswali ndani ya Ka´bah ni jambo lina sifa ya kipekee?

Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa swalah ndani ya Ka´bah ina sifa ya kipekee?

Jibu: Kama alivoswali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ina sifa ya kipekee. Kwa ajili hiyo wakati ´Aaishah aliposema kuwa anataka kuingia ndani ya Ka´bah, ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Swali maeneo pa Ismaa´iyl (حجر إسماعيل), kwa sababu ni sehemu ya Nyumba.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”

Ikafahamisha kuwa ina sifa ya kipekee, lakini ni kuhusu swalah ya kujitolea. Hakuswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) swalah za faradhi.

Swali: Inasemwa kuwa ni Sunnah ikiwepesika kufanya hivo?

Jibu: Ikiwepesika kwa ajili ya kumwigiliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23653/هل-للصلاة-داخل-الكعبة-مزية-عن-خارجها
  • Imechapishwa: 12/03/2024