Swali: Baadhi ya watuwazima hunyoa ndevu na wanaacha kidogo kwenye kidevu na wanasema kuwa hicho ndico kimezidi kwenye ngumi.

Jibu: Hili ni kosa. Kilicho wajibu ni kuziacha. Haya yamesimuliwa kutoka kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba alikuwa akifanya hivo katika ´umrah. Alikuwa akikata kile chenye kuzidi ngumi. Hata hivyo tunasema kuwa hiyo ni ijtihaad yake – Allaah amuwie radhi. Ameenda kinyume na Sunnah kwa sababu ya ijtihaad yake. Si mwenye kupatia. Maoni ya sawa ni kuwa sio Hadiyth. Yamepokelewa kutoka kwa Ibn ´Umar kutoka katika matendo yake. Kusema kwamba alikuwa akikata ndevu zake ni Hadiyth dhaifu ambayo haikusihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anapunguza. Bali yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiziachia na kuzifuga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22653/ما-حكم-من-يحلق-اللحية-ويترك-الذقن-فقط
  • Imechapishwa: 12/07/2023