Swali: Baadhi ya wanafunzi wanaona uzito kusema “imamu an-Nawawiy” kwa sababu imamu ni yule anayefuatwa.

Jibu: Hapana vibaya, anayo makosa. Anaitwa imamu. Anafuatwa katika elimu, fadhilah zake na uelewa wake. Anayo makosa. Allaah amsamehe yeye na sisi. Ni maimamu wachache wasiokuwa na makosa. Kila mwanadamu ni mwenye kukosea.

Swali: Ibn Hajar na an-Nawawiy ni katika Ashaa´irah?

Jibu: Hapana. Wamepindisha maana baadhi tu ya sifa za Allaah. Sio Ashaa´irah moja kwa moja. Wamepindisha maana baadhi tu ya sifa za Allaah na baadhi ya makosa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22644/ما-القول-في-اغلاط-النووي-وابن-حجر
  • Imechapishwa: 12/07/2023