Kuchinja baada ya mshtuko wa umeme

Swali: Makampuni ya vyakula vya kigeni huwashtua wanyama kwanza kwa mshtuko wa umeme, ambapo akapoteza fahamu, na kisha baadaye ndipo wakawachinja. Je, inafaa?

Jibu: Ikiwa kweli unajua kwamba wanafanya hivyo, usile nyama hiyo. Lakini ikiwa umesikia uvumi tu, bila ujuzi wa jambo hilo, unapaswa kutambua kuwa kimsingi ni kwamba kila kitu ni halali kukila.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 10/11/2023