Kuchelewesha josho mpaka wakati wa adhuhuri ili ahakikishe zaidi

Swali: Mwanamke damu yake imekatika kabla ya daku ambapo akanuia swawm na kujizuilia na akaoga punde kidogo kabla ya adhuhuri ili awe na uhakika zaidi kama kweli damu imekatika. Ni ipi hukumu ya funga yake?

Jibu: Ni sawa akiona kusafika usiku ambapo akafunga hata kama atachelewesha josho. Lakini haijuzu kwake kuchelewesha josho. Ni lazima kwake kuoga kabla ya jua kuchomoza ili apate kuswali Fajr ndani ya wakati wake. Akiwa anasitasita juu ya kusafika kwake basi swawm yake si sahihi. Ni juu yake kufunga. Lakini akiwa na uhakika wa kusafika mwishoni mwa usiku na akanuia kufunga, basi funga yake ni sahihi. Akiona damu basi atatakiwa kufungua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/794/فتاوى-رمضانية
  • Imechapishwa: 16/04/2023