Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kunaingia pia Swarf na ´Atwf.”

Swarf maana yake ni kumfanya mwanamke kuwa mbali na mume wake na mwanamme kuwa mbali na mke wake[1] kwa njia ya kwamba wanafanyiwa uchawi. Matokeo yake mtu akija kwa mke wake anamuona kwa umbile baya na matokeo yake anamkimbia na anakuwa hataki kumsogelea. Au kinyume chake yeye akawa anamchukia mume wake kwa njia ya kwamba anapomuona mume wake basi humuona kwa umbile baya asiloweza kustahamili hata kumtazama. Hivyo wanatengana. Hii ndio Swarf. Mchawi amefanya wanakuwa ni wenye kukimbiana licha ya kuwa uhakika wa mambo hakuna kitu kwa wote wawili. Kilichopo ni kwamba mchawi amewafanyia uchawi kwa njia ya kwamba amemfanya mwanamke amuone mume wake katika umbile baya kwa kiasi cha kushindwa hata kumwangalia. Vivyo hivyo amfanye mume katika umbile baya kwa njia ya kwamba mke wake akimtazama hastahamili kumwangalia. Hiyo inakuwa ni sababu ya kupatikana mtengano.

´Atwf ni kinyume cha Swarf[2]. Mchawi anampendezesha mwanamke kwa mwanamme kwa njia ya kwamba anamfanyia uchawi mwanaume na anakuwa ni mwenye kumili kwa mwanamke. Aidha anampendezesha mbele ya macho yake ijapokuwa atakuwa ni mbaya na mwenye maumbile mabaya. Pamoja na hivyo mbele ya macho yake hakuna mzuri amuonaye kama yeye. Vilevile mchawi akimfanyia uchawi mwanamke kwa hali ya kwamba pale anapomtazama mume wake hakuna mzuri amuonaye kama yeye ijapokuwa atakuwa mbaya na mwenye maumbile mabaya. Hii ndio inaitwa ´Atwf. Amempendezesha mwanamke kwa mwanamke na kinyume chake. Hii ni aina moja wapo ya uchawi.

Miongoni mwa uchawi kunaingia vilevile at-Tiwalah. Ni kitu au dawa inayofanywa na mchawi kisha wanampa mume au mke ambacho wanadai kuwa inampendezesha mwanamke kwa mumewe na mwanaume kwa mkewe. Yule mwenye kufanya au akawa radhi na uchawi, basi anakuwa kafiri kwa dalili ya Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ

“Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili [katika mji wa] Baabil; Haaruut na Maaruut. Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi]”.”

Kwa hivyo mwenye kufanya uchawi, akajifunza nao, akaufunza au akawa radhi nao – ikiwa ni pamoja vilevile na Swarf na ´Atwf – basi anakuwa kafiri kwa sababu amemshirikisha Allaah (´Azza wa Jall). Dalili ni Aayah zifuatazo:

وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ

“Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi]”.”

فَيَتَعَلَّمُونَ مِنْهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِ بَيْنَ الْمَرْءِ وَزَوْجِهِ

“Basi wakajifunza kutoka kwa hao [Malaika] wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo kati ya mtu na mkewe.”

وَمَا كَفَرَ سُلَيْمَانُ وَلَـٰكِنَّ الشَّيَاطِينَ كَفَرُوا يُعَلِّمُونَ النَّاسَ السِّحْرَ وَمَا أُنزِلَ عَلَى الْمَلَكَيْنِ بِبَابِلَ هَارُوتَ وَمَارُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنْ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَا إِنَّمَا نَحْنُ فِتْنَةٌ فَلَا تَكْفُرْ

“Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili [katika mji wa] Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi].”[3]

Lakini itambulike kuwa mchawi hawezi kumdhuru yeyote isipokuwa pale ambapo Allaah (´Azza wa Jall) atakadiria dhara hilo kwa mtu huyo. Hapo ndipo madhara yatatokea. Amesema (Ta´ala):

وَمَا هُم بِضَارِّينَ بِهِ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ

“Na wao si wenye kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah.”[4]

Hapa kunamaanishwa idhini ya Allaah ya kilimwengu na ya kimakadirio.

[1] Tafsiyr Ibn Kathiyr (01/144) na “Faydhw-ul-Qadiyr” (02/408)

[2] an-Nihaayah fiy Ghariyb-il-Hadiyth (01/200)

[3] 02:102

[4] 02:102

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 15/04/2023