Kuanza kufunga siku sita za Shawwaal wakati wa mchana

Swali: Je, ni sharti kulaza nia katika swawm ya siku sita za Shawwaal?

Jibu: Ndio, kwa njia ya ubora. Vinginevyo hapana neno iwapo atafunga kuanzia wakati wa mchana. Lakini swawm yake haiwi kamili isipokuwa pale atakapolaza nia. Katika hali hiyo funga yake inakuwa kamili. Vinginevyo swawm inakuwa pungufu akifunga kuanzia wakati wa mchana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21735/ما-حكم-تبييت-النية-في-صيام-ست-شوال
  • Imechapishwa: 05/05/2022