Kuunganisha deni la Ramadhaan na swawm ya Shawwaal

Swali: Nimesikia kuwa haifai kwa mfu kuunganisha swawm ya kulipa deni (صوم القضاء) na swawm ya sunnah? Kwa msemo mwingine ni kwamba ikiwa mtu anadaiwa baadhi ya siku za Ramadhaan ambapo alikula kutokana na udhuru unaokubalika katika Shari´ah kisha akazilipa katika mwezi wa Shawwaal na baadaye akataka kufunga siku sita za Shawwaal basi haifai kwake akaunganisha funga hii na ile nyingine. Anachotakiwa kufanya ni kula angalau siku moja. Je, maneno haya ni kweli?

Jibu: Sijui msingi wowote wa hayo uliyoyataja. Usawa ni kwamba hapana ubaya kufanya hivo kutokana na kuenea kwa dalili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/396)
  • Imechapishwa: 05/05/2022