Swali: Unasemaje juu ya maneno ya Imaam Ahmad:

”Mwenye kuacha Witr kwa kuendelea ni mtu fasiki”?

Jibu: Alisema kuwa ni mtu muovu. Hii ni Ijtihaad yake. Witr sio lazima. Bali ni Sunnah inayokokoteza na sio lazima. Hata hivyo maneno yake si sahihi kwa upande wa dalili za Kishari´ah.

Swali: Mtu akiiacha anakuwa mwenye kutenda dhambi?

Jibu: Hapana, si mwenye kupata dhambi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipomfunza bwana mmoja swalah tano bwana huyo alimuuliza:

”Je, kuna nyenginezo zinazonilazimu, ee Mtume wa Allaah?” Akamwambia: ”Hapana, isipokuwa ukijitolea.””

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21926/حكم-الخلوة-بالمحرم-الذي-لا-يخاف-الله
  • Imechapishwa: 12/01/2023