Kimsingi ni kufaa vichinjwa vya watu wa Kitabu, lakini…

Swali: Ni ipi hukumu ya kula nyama zinazoletwa kutoka nje katika nchi za manaswara na ambazo hatujui zimechinjwa namna gani?

Jibu: Kimsingi ni kwamba vichinjwa vya watu wa Kitabu ni halali. Hilo ni kwa nukuu ya Qur-aan. Hata hvyo msingi huu unakinzana na uchinjaji wao usiokuwa wa Kishari´ah, ima wawaue kwa maji ya moto au kwa kutumia mashine zenye kukata shingo. Huku sio kuchinja. Hazikukusudia wala wanyama hawakuchinjwa kwa kutajiwa jina la Allaah kwa kila mmoja. Huu ni uchinjaji wa pamoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 12/10/2023